On 4:44 AM by AFRIKA SHANGWE No comments
ARTIST-Joh maker ft Stamina
SONG- wanasemaje
STUDIO- Kwanza records
PRODUCER- Vennt skillZ
SONG WRITER -Joh maker and Stamina
INTRO (stamina)
yeah kwanza records vennt i see you bro
shorwebwenzi on this one joh maker make it hapen
VERSE 1 (joh maker)
usifiche siri achia wazi,rudia mara mbili.
kama hauna dili usiachie ngazi,kamia namba mbili.
haya sio maneno mema,bali mema ni mahubiri.
nani aliyekwambia wema,hajapitia kuvaa kandambili?.
nlitwaaga nyota kule dar,moro usiniite bosi.
joh maker MC mwenye njaa,nashiba mi nkiona mic.
vunja church jenga bar,upate ustar wa magazeti.
ficha nyeti,nasikia unaziachaga wazi ukiona senti.
sili nyama mi mifupa,na usiniite fisi.
ninacho cha kukupa,sio tamaduni ila vitu halisi.
sio kampuni wala duka,kipi unachohisi.
hii biashara mtaji kichwa.njoo ujaribu kuufilisi.
kama utanipata sawa,sawa data na madawa.
msouth hata ukibana vipi,mbongo pipi kama kawa.
sio muhaya anavyopaa,ulaya kama anambawa.
niko tabora unyamwezini,black america kama kawa.
ni mazishi,daktari anakupa nnapona mimi.
hata uwe mbeya vipi,huwezi jua siri ya kaburini.
sikuizi mtoto sio wa mama,bali ni mtoto wa mjini.
kaa ukizini we utakufa,njoo upate ajali na mimi.
CHORUS (joh maker and stamina)
WANASEMAJE
eti braza umechezea bahati hata ukitoka tena huwezi shine mitaa ya kati
WANASEMAJEEE
we supa nyota haikukufaa sio handsome wala hufai kabisa kuwa staa
WANASEMAJE
mtaani unapozi nyingi hata uchane vipi huwezi kuwa selemani msindi
WANASEMAJEEE
acha mziki rudi shule maana kila unachofanya kwako naona kazi bure
VERSE 2 (Stamina)
kisa sio mrefu wananisema,ingekuaje ningeumbwa chongo.
wajui ufupi sio kilema,ndo maana sitembelei magongo.
nipe noti bandia,nikupe bukula ya halali.
wananiita MC ngamia,maana nna nundu la mistari.
hata nikikata ringi,mdomoni siishiwi madini.
acha wafate misingi,ila hela nitazifata mimi.
maaMC wengi wafu,wamekufa kwa ugonjwa wa promo.
wanasema wana level chafu,mbele yangu mtumiaji wa omo.
wananiita kiungo kuntu,nawalisha kila mechi.
hawa maforward butu,hawapangwi wanasotea benchi.
refa mkunja ndita,uwanjani sinaga fair.
siko base niko twitter,nifollow tuweze kushare.
AAH habari zao sina,zangu wanazo kuwa mi mkali.
wamepauka kivina,wanachovya hadi mistari.
mi ni bosi wa zumo,daily macho kwenye pesa .
eti mjini msingi kiuno,angalieni msiishie madancer.
niko deep,ninazip kila mingo.
wajinga wanaleta bif,navyocliff kwa mitindo.
mabishoo hali duni,ndo maana wanapenda vya dezo.
nishafanya kila uhuni,hadi kuvaa kondomu mlegezo.
CHORUS (joh maker and stamina)
WANASEMAJE
eti braza hujui kuchana hawaelewi kabisa mziki gani we unafanya
WANASEMAJEEE
haujawahi kuwaimbia wasichana kama umeshindwa game rudi mgeta ukauze nyanya
WANASEMAJE
rapa gani mfupi kama wewe umefanana na kuku juzi ulikoswa na mwewe
WANASEMAJEEE
bora uache mziki urudi moro hii fani hauiwezi kasimamie vigodoro
VERSE 3
stamina
machinga nliopitia depo,sitishwi na mgambo wa jiji.
sharo ukifata upepo,utarudi kwenu kimbiji.
wanaitana mapunga,ila wote ni bokoboko.
wanavina vya kuungaunga,utasema wanaaindikia royco.
joh maker
yooh usiniite ney wa mitego we ni mchelemchele
verse inamitego haihitaji mashoga wakae mbele
bado si tupogo zaidi ya ommy mwenye dimpo
nagawa vipigo daima mi sigomi kwenye witoo
stamina
nakula unga ila sembe,south sipigi mbizi.
mi ndo genious wa milembe,niliyefeli ule mtihani wa uchizi.
mjeshi nisiye na gwanda,kuluta utaeleza kipi.
wanauliza jogoo la shamba,huku mjini nawika vipi
joh maker
yanukuu mema japo mi na mengi ya kusema
mko wengi ila maker mi natenzi za kuchana
mi naujenzi wa kunena pastor mwenye mema
na kama ukitaka elimu mi ndo shule ya kusoma
CHORUS (joh maker and stamina)
WANASEMAJE
we supa nyota haikukufaa sio handsome wala hufai kabisa kuwa star
WANASEMAJEEE
rapa gani mfupi kama wewe umefanana na kuku juzi ulikoswa na mwewe
WANASEMAJE
acha mziki rudi shule maana kila unachofanya kwako naona kazi bure
WANASEMAJEEE
bora uache mziki urudi moro hii fani hauiwezi kasimamie vigodoro
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Search
.
Hot Posts
-
ARTIST -Joh maker ft Stamina SONG - wanasemaje STUDIO - Kwanza records PRODUCER - Vennt skillZ SONG WRITER - Joh maker and...
SHXNGWE. Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment